Nukuu Papo Hapo na Arifa

Maoni elfu 269
Daraja la maudhui
Miaka 3 kwenda juu
1B+
Vipakuliwa
Daraja la maudhui
Miaka 3 kwenda juu
Pata maelezo zaidi
Picha ya skrini
Picha ya skrini
Picha ya skrini
Picha ya skrini
Picha ya skrini
Picha ya skrini

Kuhusu programu hii

Programu ya Nukuu Papo Hapo na Arifa kuhusu Sauti huwawezesha viziwi na watu walio na matatizo ya kusikia kufanya mazungumzo ya kawaida na kusikia sauti zinazowazingira kwa urahisi zaidi, ukitumia tu simu yako ya Android.

Kwenye vifaa vingi, unaweza kufungua programu ya Nukuu Papo Hapo na Arifa kuhusu Sauti kwa kufuata hatua hizi:
1. Fungua programu ya Mipangilio kwenye kifaa chako
2. Gusa Ufikivu
3. Kulingana na kipengele ambacho ungependa kutumia, gusa Nukuu Papo Hapo au Arifa kuhusu Sauti

Unaweza pia kutumia kitufe cha zana za ufikivu, ishara au Mipangilio ya Haraka ili uanzishe Nukuu Papo Hapo au Arifa kuhusu Sauti (https://g.co/a11y/shortcutsFAQ).

Unukuzi katika wakati halisi
• Kiolesura cha mazungumzo kilichobuniwa upya hutoa mawasiliano rahisi na laini zaidi ya kawaida.
• Pata unukuzi katika wakati halisi katika zaidi ya lugha na lahaja 80. Weka maneno maalum unayotumia mara kwa mara, kama vile majina au bidhaa za nyumbani.
• Weka simu yako katika hali ya kutetema mtu anapotamka jina lako.
• Andika majibu katika mazungumzo yako.
• Tumia maikrofoni za nje zinazopatikana katika vifaa vya sauti vyenye waya, vifaa vya sauti vya Bluetooth na maikrofoni za USB kupokea sauti vizuri zaidi.
• Kwenye simu za kukunja, onyesha manukuu na majibu yaliyoandikwa kwenye skrini ya nje ili iwe rahisi kuwasiliana na wengine.
• Chagua kuhifadhi manukuu kwa siku 3. Manukuu yaliyohifadhiwa yatasalia kwenye kifaa chako kwa siku 3 ili uweze kuyanakili na kuyabandika kwingineko. Kwa chaguomsingi, manukuu hayahifadhiwi.

Arifa kuhusu Sauti
• Pata arifa kuhusu sauti muhimu karibu nawe, kama vile king'ora cha moshi kinapolia au mtoto anapolia.
• Weka sauti maalum ili upate arifa vifaa vyako vinapolia.
• Kagua sauti kutoka saa 12 zilizopita ili usikie kilichofanyika karibu nawe.

Mahitaji:
• Android 12 na matoleo mapya zaidi

Programu ya Nukuu Papo Hapo na Arifa kuhusu Sauti imeundwa kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Gallaudet, chuo kikuu cha Viziwi na watu wenye matatizo ya kusikia kinachoongoza nchini Marekani.

Usaidizi na maoni
• Ili kutoa maoni na kupata taarifa kuhusu bidhaa, jiunge na Kikundi cha Ufikivu kwenye Google kupitia https://g.co/a11y/forum
• Ili kupata usaidizi wa kutumia Nukuu Papo Hapo na Arifa kuhusu Sauti, wasiliana nasi kupitia https://g.co/disabilitysupport

Ilani ya ruhusa
Maikrofoni: Programu ya Nukuu Papo Hapo na Arifa kuhusu Sauti inahitaji kufikia maikrofoni ili kunukuu matamshi na sauti zilizo karibu nawe. Sauti haihifadhiwi baada ya manukuu au sauti zinazotambuliwa kuchakatwa.
Arifa: Vipengele vya Arifa kuhusu Sauti vinahitaji ruhusa ya kufikia arifa ili kukuarifu kuhusu sauti.
Vifaa vilivyo karibu: Programu ya Nukuu Papo Hapo inahitaji ruhusa ya kufikia vifaa vilivyo karibu ili kuunganisha na maikrofoni zako za Bluetooth.
Huduma ya Ufikivu: Arifa kuhusu Sauti hutumia API ya Huduma za Ufikivu ili kutekeleza huduma yake ya utambuzi wa sauti chinichini na kuwezesha ufikiaji wa haraka kupitia Kitufe cha zana za ufikivu au mguso wa kifaa chako. API hii haitumiwi kusoma, kukusanya wala kuhifadhi maudhui yaliyo kwenye skrini au taarifa binafsi.
Arifa za matukio yenye sauti na manukuu ya mazungumzo yako kwa wakati halisi
Ilisasishwa tarehe
17 Ago 2026

Usalama wa data

Usalama huanza kwa kuelewa jinsi wasanidi programu wanavyokusanya na kushiriki data yako. Faragha ya data na mbinu za usalama zinaweza kutofautiana kulingana na matumizi yako, eneo ulilopo na umri wako. Msanidi programu ametoa maelezo haya na anaweza kuyasasisha kadiri muda unavyopita.
  • Hakuna data inayoshirikiwa na wengine
    Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi wasanidi programu wanavyobainisha kushiriki data
  • Programu hii huenda ikakusanya aina hizi za data
    Taarifa binafsi, Sauti na nyingine3
  • Data inasimbwa kwa njia fiche inapotumwa
  • Data haiwezi kufutwa

Ukadiriaji na maoni

Maoni elfu 264

Vipengele vipya

• Kiolesura cha mazungumzo kilichobuniwa upya hutoa mawasiliano rahisi na laini zaidi ya kawaida.